Keezywear Editor Keezywear Editor Author
Title: Kanisa Lakataa Kumbatiza Mtoto wa Aunty Ezekiel Kwa Sababu Hii...
Author: Keezywear Editor
Rating 5 of 5 Des:
Kanisa Katoliki limemzuia staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel kumbatiza mwanaye kutokana na kutokidhi matakwa ya kanisa. Tukio hilo lime...

Kanisa Katoliki limemzuia staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel kumbatiza mwanaye kutokana na kutokidhi matakwa ya kanisa.

Tukio hilo limetokea hivi karibuni mara baada ya mwigizaji huyo ambaye imani yake ni ya Kiislamu, kutaka kumbatiza mwanaye huyo ambaye baba yake ( Moze Iyobo) ni Mkatoliki.

“Alikuwa amejipanga kumbatiza Kikristo kutokana na imani ya baba mtoto wake lakini alipokutana na padri Paul Ruwaaich wa Parokia ya Uparo Moshi aliyekuwa Dar kikazi akamtaka akaanzie kusali kwenye Jumuiya Ndogondogo (mtaani kwake), abadilishe dini ndipo mtoto huyo abatizwe kwani ndizo taratibu za Kanisa Katoliki.

“Alipopewa sharti hilo, lilikuwa gumu kwa Aunt, ikabisi ageuze zake,” Aunt alipoulizwa  kuhusu suala hilo, alisema amebaki njia panda na anatafakari cha kufanya.

Author

Advertisement

 
Top