Keezywear Editor Keezywear Editor Author
Title: Diamond azungumzia mtoto wake na Zari, Collabo na Ludacris, Tuzo za MTV na mengine mengi
Author: Keezywear Editor
Rating 5 of 5 Des:
Moja ya Watangazaji wenye majina makubwa East Africa ni Mtangazaji kutoka Citizen TV na Radio, Nairobi Kenya, Mzazi Willy Tuva, ambaye alipa...
Moja ya Watangazaji wenye majina makubwa East Africa ni Mtangazaji kutoka Citizen TV na Radio, Nairobi Kenya, Mzazi Willy Tuva, ambaye alipata nafasi ya kufanya Exclusive Interview na Diamond Platnumz, majibu yake kwenye maswali kadhaa yako hapa:

Hili ni jibu kuhusu Zari kujifungua:
‘Zari kujifungua in the next 3 weeks’

Hapa kuna majibu pia kuhusu jina la mtoto wake na mpenzi wake Zari:
‘Mtoto wangu atazaliwa Tanzania, jina lake bado tunajadiliana na mamake, Mimi nasema aitwe Candy, mamake anasema aitwe Zara’

Kajibu pia kilichomfanya ampende zaidi Zari:
‘Mwanamke ambae amekubali kunizalia nampa heshima sana, Nimekutana na Wanawake lakini wengi waliniambia ngoja ngoja kama vile nilivyoimba kwa wimbo wangu Nikifa Kesho ukizingatia ni Mwanamke maarufu, kiukweli Zari kunizalia imenifanya nimpende Sana’

Collabo na Ludacris?
‘NANA ambayo nilifanya na MR. FLAVOUR ilikuwa nifanye na msanii wa Marekani, LUDACRIS’

Kusitisha collabo za nje ya TZ:
‘I was misquoted, sijasitisha kufanya Collabo na wasanii wa Nigeria ila tu tumepunguza maana sasa hivi nafanya kazi na wasanii wa pande zote za Afrika, Juzi nimefanya na Donald wa Afrika Kusini na pia nyingine nimefanya na Msanii wa Congo’

Collabo na wasanii wa Kenya je?
‘Kuhusu kufanya collabo na @bahatikenya na @willypaulmsafi, @diamondplatnumz Amesema kuimba Gospel itakua tatizo maana ni muislamu labda wimbo ikawa ni neutral maana hataki kuonekana kama anachokoza dini ila anawakubali sana’

Kuna collabo na Wakenya inakuja?
‘Muda si mrefu tutafanya kazi na @jaguarkenya na @collinsmajale. Namkubali @chikuzee_kenya pia ilikuwa nifanye kazi naye lakini aliyekuwa anamdhamini alipotea...lakini hivi karibuni inshallah tutafanya kazi moja kubwa na msanii wa Kenya ambaye itatusua Afrika Nzima’

Anaitamani Siasa?
‘In future ningependa kuja kuwa Waziri wa Michezo hata nishaambia Mamangu sana ila si kwa sasa hivi’

Ana matumaini na Tuzo za MTV MAMA:
‘Ukiangalia ile hashtag ya MTV MAMA kwa mitandao East African tuko mbele. Sijui ila tunaweza tukachukua tuzo zote maana, wasipo tupa tuzo yeyote itabidi niwaulize wanaangalia vigezo gani ikija kwenye maswala ya kupeana Tuzo’

Kafungukia tena kuhusu kilichofungua milango ya mafanikio yake:
‘Siri ya mafanikio, uvumilivu, discipline, na kumwomba Mwenyezi Mungu, hauwezi kufanikiwa bila kutokea vikwazo’

Hayo ni baadhi ya maswali ambayo msanii huyo wa Bongoflava aliulizwa kwenye Interview hiyo. Endelea kutembelea Keezywear.com ili kufatilia Interviews mbalimbali za wasanii wakubwa!!

Author

Advertisement

 
Top