Keezywear Editor Keezywear Editor Author
Title: Baadhi ya Wasanii wa Bongo Movies Wazindua Kampeni ya ‘Mama Ongea na Mwanao’
Author: Keezywear Editor
Rating 5 of 5 Des:
Siku ya jana, Agosti 20 wasanii kutoka kwenye tasnia ya filamu nchini, Steve Nyerere, Wema Sepetu, Batuli, Snura, Wastara na wengineo ...

Siku ya jana, Agosti 20 wasanii kutoka kwenye tasnia ya filamu nchini, Steve Nyerere, Wema Sepetu, Batuli, Snura, Wastara na wengineo wamezindua kampeni mpya iitwayo Mama Ongea Na Mwanao.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kampeni hiyo Steve Nyerere akizungumza na waandishi wa habari alisema…‘Mimi kama Mwenyekiti wa Mama ongea na mwanao ni kwamba hii Mama ongea na mwanao nadhani mmeona tangu tumepata uhuru nchi yetu haijawahi kuwa na makamu urais mwanamke hii ni historia kwa Tanzania mimi na imani ni kumuenzi mwanamke nani kama Mama na imani wa Mama wote  watampigia kura mama mwenzao ili tushinde kura kwa kishindo.
Mama Samia Suluhu kama anavyojulikana ni mfanyakazi hodari, mchapakazi na ameweza kuwa katika bunge la katiba ambalo limechanganyikana watu mbalimbali na aliweza kulithibitisha vizuri lakini vile vile tuna John Pombe Magufuli ni mtu ambaye mchapakazi, hodari hatuhitaji umaarufu wa mtu tukisema umaarufu wa mtu hata Diamond anajaza watu, hata Alikiba anajaza, watu hata sisi tulio hapa mbele zetu tunajaza watu nia tunahitaji Rais, Rais hahitaji kujaza watu bali Rais anahitaji kutatua matatizo ya watanzania tiba mbadala wa mama zetu wanapata Elimu na vitu mbalimbali – Steve Nyerere.
Kwa hiyo sisi kama wasanii tunavyojiita ni kioo cha jamii tunasema kwamba Mama ongea na Mwanao mwanamke akipewa nafasi anaweza na mimi ninaamini hata katika mchakato wa kumpata mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi  wanawake waliingia watatu mwanaume ni mmoja hii ni kuonesha jinsi gani Mwanamke anapata nafasi kubwa katika Uongozi  wa taifa hili la leo na kesho – Steve Nyerere.

Chanzo: millardayo.com

Author

Advertisement

 
Top