Mtalam III Mtalam III Author
Title: Inasemekana Jokate alienda kumtambulisha Ali Kiba kwao, hiki ndo kilichotokea...
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Imevuja! Gumzo la ndoa ya staa mwenye jina kubwa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Mbongo-Fleva Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ inadaiwa kup...
Imevuja! Gumzo la ndoa ya staa mwenye jina kubwa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Mbongo-Fleva Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ inadaiwa kupigwa zengwe kama ilivyowahi kutokea kwa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kufuatia madai ya mwanadada huyo kumtambulisha jamaa huyo kwao kisha kukataliwa.

MINONG’ONO:
Habari kutoka chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao, tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo wawili hao walihudhuria kwenye harusi ya dada wa Jokate hivyo kuibua minong’ono kwamba huenda harusi inayofuata itakuwa yao.

Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, habari mbaya ni kuwa baada ya Jokate kumtambulisha Kiba kwa ndugu, jamaa na marafiki baadaye kumpeleka kwao, wazazi wa mwanadada huyo walikuja juu wakidai jambo hilo haliwezekani huku sababu nne zikianikwa.

KIGEZO CHA DINI:
Madai yalishushwa kuwa, sababu ya kwanza ni kwamba, familia ya Jokate hasa wazazi wake ni watu walioshika sana Dini ya Kikristo (Kanisa Katoliki) huku Kiba akiwa ni Muislam kama ilivyokuwa kwa Diamond aliyeshindwa kumuoa Jokate kwa kigezo hichohicho.

NDOA ZA MASTAA NI TATIZO?
Ilidaiwa kuwa, sababu ya pili iliyotolewa na wazazi hao ni kwamba, hawataki binti yao kuolewa na msanii mwenzake kwa kuwa wanajua ndoa za mastaa zinavyokuwa na ‘drama’.

KIGEZO CHA KABILA:
Kigezo kingine kilichotajwa ni kabila ambapo wazazi hao wanataka Jokate aolewe na mtu wa kabila lake la Wangoni tofauti na Kiba ambaye ni Muha.

KIGEZO CHA BONGO FLEVA:
Chanzo kilikwenda mbali zaidi na kudai kuwa, wazazi hao wanaamini kwamba baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva ni wahuni hivyo kuwawia vigumu kukubali binti yao kuolewa na Mbongo-Fleva.Pia habari za ndani zilidai kwamba, Jokate na Kiba walikuwa kwenye harakati za kuoana kabla ya mwaka huu kumalizika ila zengwe limekuwa kubwa upande wa familia hasa kwenye suala la dini ambapo kila mmoja amekuwa akitaka mwanaye abadili dini.

KAMA DIAMOND:
“Unajua kilichompata Kiba ni kama kile kilichomfika Diamond kipindi kile alipotaka kumuoa Jokate. Ilikuwa ni ishu hiyohiyo ya dini maana wazazi wa Jokate walikuwa wakimwambia kila siku kama kweli anampenda mtoto wao basi abadili dini lakini Diamond hakuweza kufanya hivyo na kujikuta wakishindwa kufikia lengo la kufunga ndoa,” kilitambaa chanzo hicho.

KIBA KAMA KAWA:
Kama kawaida yake, Kiba alipoulizwa juu ya ishu hiyo alikanusha vikali akidai kwamba hajawahi kuwa na mipango hiyo na mrembo huyo.
“Ulishawahi kunisikia nikizungumzia ishu hiyo? Siyo kweli bwana…hakuna kitu kama hicho,” - Ali Kiba
alisema Kiba akionekana ‘kumaindi’ kwa kuulizwa juu ya jambo hilo.Kwa upande wake Jokate hakupatikana hewani na hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.

TUJIKUMBUSHE:
Kwa muda mrefu, Jokate na Kiba wamekuwa wakiripotiwa kuwa ni wapenzi lakini Kiba amekuwa mstari wa mbele kukanusha huku Jokate akikiri kuwa jamaa huyo ni mtu wake.

Chanzo: GPL.

Author

Advertisement

 
Top