Mtalam III Mtalam III Author
Title: Hivi Zari amemfata Diamond Nigeria?
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Je, ile Project ya Diamond na Zari inaendelea? Ndo swali ambalo mwandishi Sandu wa Bongo5 amejaribu kuuliza baada ya mrembo huyo wa Uganda ...
Je, ile Project ya Diamond na Zari inaendelea? Ndo swali ambalo mwandishi Sandu wa Bongo5 amejaribu kuuliza baada ya mrembo huyo wa Uganda kupost picha akiwa kwenye ndege.
 Diamond na Zari

Wote tunafahamu kwamba Diamond yupo Nigeria sasa akijipanga kudondosha bonge la Show kwenye tukio la ugawaji wa tuzo za michezo, Glo­CAF Awards. Bongo5 wameandika hivi:

Licha ya kuwa Diamond Platnumz hakuongozana na mpenzi wake Zari The Boss Lady kwenda Nigeria Jumatatu hii, lakini kuna uwezekano mkubwa wawili hao wakawa pamoja kwenye hafla ya ugawaji tuzo za michezo za Glo­CAF Awards itakayofanyika Alhamisi Jan 8 jijini Lagos, ambapo Platnumz ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza.
 


Zari The Boss Lady amepost picha (hapo juu) asubuhi ya leo Jumatano (Jan 7) akiwa kwenye ndege na kuandika “Another day, another flight. Stay blessed”, inayoashiria kuna uwezekano mkubwa akawa anaenda kwa baby wake Nigeria. 


Diamond naye jana alipost picha zake mwenyewe (hapo juu) akiwa anaonekana mpweke na kuandika, “Kuna mtu alikuwa mnyooonge na mpweke jana…” inamaanisha mtu muhimu ambaye ni baby wake ndiye anayekosekana.

Baada ya kuwa pamoja Uganda kwenye party ya Zari mwishoni mwa mwaka jana, Zari na Diamond walisafiri pamoja kwenda Burundi na Rwanda na ndio sababu kuna kila dalili pia watakua pamoja Nigeria licha ya kuwa hawakusafiri pamoja.”

Source: Bongo5.

Author

Advertisement

 
Top