Mambo yanazidi kuwa mazuri mwaka huu wakati tunategemea wasanii wengi kutoa ngoma kali kama ilivyokuwa mwaka jana. Baadhi ya wasanii washaanza kutease, kuachia snippet na artwork za nyimbo zao zinazokuja.
Kwa upande wa Ommy Dimpoz, yeye kashafanya collabo moja na Avril kutoka Kenya. Pia kupitia Millardayo nimepata kujua kwamba mkali huyo ameingia Studio kufanya ngoma na wakali wengine kutoka Kenya. Mtandao huo umeandika hivi:
“Omary Faraji Nyembo aka Ommy Dimpoz ambaye bado yuko Nairobi kiziara, time hii ameingia studio na kundi la Sauti Sol kurekodi single mpya.
Kupitia kwenye Instagram, Sauti Sol wamepost picha saa kadhaa zilizopita (jana) na kuandika;
“Late night #studiothings in Nairobi with our Tanzanian brother @ommydimpoz Always great to connect!! #TeamSautiSol Muziki moto iko jikoni!!!! 2015 work!!!” – @sautisol
Sauti Sol ni wakali kutoka Kenya, ambao moja ya nyimbo yao inayofanya vizuri sasa hivi ni Sura Yako.”
Source: Millardayo.