Mtalam III Mtalam III Author
Title: Hii sasa kali: Unajua alichokisema Nay wa Mitego baada ya Nikki Mbishi kutangaza kuacha muziki?
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Juzi kati msanii wa Hiphop, Nikki Mbishi alitangaza kuacha kufanya Muziki kwa madai kwamba haumlipi. Walijitokeza baadhi ya wasanii kama P...
Juzi kati msanii wa Hiphop, Nikki Mbishi alitangaza kuacha kufanya Muziki kwa madai kwamba haumlipi. Walijitokeza baadhi ya wasanii kama Prof. Jay na Chid Benz ambao walimuomba aendelee kufanya kwasababu game inahitaji watu kama yeye.

Mtandao wa Sammisago umetoa info kuhusu kauli ya Nay wa Mitego baada ya kusikia mbaya wake (Nikki Mbishi) kaamua kuacha Muziki. Sammisago imeandika ifuatavyo:

“Kupitia exclusive interview na Power Jams, Nay wa Mitego amezungumzia hatua ya Nikki Mbishi ya kuacha muziki na kusema “Ukiona kitu hakikulipi ni bora uachane nacho, mtu anaweza kuangalia kitu na kujua hakimfai na bora afanye mambo mengine,” 

Nay aliendelea kusema, “Sijui kwanini amechelewa, nimefurahi kuona maamuzi mazuri kijana mwenzangu aliyofanya, amejitambua na kuamua kuangalia vitu vingine, niko tayari kumshauri kama bado hajapata cha kufanya”.

Ikumbukwe jamaa hawa wawili walikuwa kwenye ugomvi mpaka Nikki Mbishi aliamua kuandika wimbo alioupa jina Nay wa Mitego hahaaa!

Source: Sammisago.

Author

Advertisement

 
Top