Mtalam III Mtalam III Author
Title: Ben Pol amepanga kufanya makubwa mwaka huu
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Wakati kashaanza kufanya amsha amsha za kuachia wimbo wake mpya unaoitwa Sophia, January 15, msanii Ben Pol ana mipango mikubwa sana mwaka...
Wakati kashaanza kufanya amsha amsha za kuachia wimbo wake mpya unaoitwa Sophia, January 15, msanii Ben Pol ana mipango mikubwa sana mwaka huu wa 2015.
Ben Pol

Kupitia mtandao wa Bongo5 ambao umeandika mipango ambayo Ben Pol amedhamiria kuifanya kwa mwaka huu, nimeona sio mbaya wewe kama shabiki wa mkali huyo wa RnB kuyajua haya. Bongo5 wameandika hivi:

Hitmaker wa ‘Unanichora’ Bernard Paul aka Ben Pol, amesema malengo yake ya mwaka 2015 ni kulifikia soko la ushindani la kimataifa katika muziki wa kizazi kipya, kunyakua au kuwa nominated katika tuzo za kimataifa pamoja na video za nyimbo zake kuchezwa katika runinga za kimataifa.

“Bado tunaendelaa kupambana , bado tunaendelea ku­push kazi naamini siku moja Mwenyezi Mungu nitakuja kutokezea sehemu,” Ben Pol alikiambia kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya. 

“Kwahiyo tayari nimeanza kutumatuma nyimbo kama kwa mwaka jan nimeweza kufanikiwa kwa kiasi fulani mpaka kupata nomination kwenye tuzo za AFRIMMA, kupata airtime kwenye international TV stations, kwahiyo taratibu ninaendelea,” ameongeza. 

 “Mwenyezi Mungu akijaalia mwaka huu tena nitapanua network kidog na kufanyafanya collabo na wasanii wa kimataifa vitu vikiwa onset nafikiri tutapean taarifa.” alimaliza.”

Source: Bongo5.

Author

Advertisement

 
Top