Producer wa Classic Sounds, Mona Gangstar amejitokeza kulalamika tabia ya msanii aliye chini ya label yake, Young Killer (Msodoki) kwamba sasa amebadilika na kwamba hamuheshimu tena.
Kipindi cha nyuma zilizuka taarifa kwamba kuna kutoelewana kati ya Young Killer na producer huyo. Akiongelea swala hilo na SamMisago.com, Mona Gangstar alisema:
“Young Killer amebadilika, amekuwa maarufu na ameshikwa masikio na watu, Bado nina mkataba na Young Killer mpaka December 2014 ila anaukiuka mkataba huu kwa kwenda kufanya kazi studio zingine na sasa hata Classic Sounds hafiki.
Classic Sounds haimbani msanii ila akitaka kufanya kazi nje ya studio hii ni lazima tubaki kama Executive Producer wa kazi hio ilituhakikishe kiwango cha kazi ni bora, Young Killer amefanya kazi nje ya studio bila taarifa wakati mkataba wa Classic Sounds hauruhusu hicho kitu” Alisema Monaganster.