Mtalam III Mtalam III Author
Title: Mpigie kura Cindy Rulz ashinde tuzo ya UMA’s kwenye kipengele cha ‘Best International Artist’
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Rapper wa kike kutoka Tanzania, Cindy Rulz, ametajwa kuwania tuzo za Underground Music Awards, UMA’s za Marekani. Cindy Rulz Tuzo z...
Rapper wa kike kutoka Tanzania, Cindy Rulz, ametajwa kuwania tuzo za Underground Music Awards, UMA’s za Marekani.
Cindy Rulz

Tuzo za UMA’s ni kubwa zaidi Marekani zinazolenga kuwatunza wasanii, waandishi wa nyimbo na watayarishaji wa muziki wanaojitegemea (wasio chini ya label) nchini Marekani.

Cindy Rulz ni msanii pekee wa Afrika aliyetajwa mwaka huu kuwania tuzo hizo kwenye kipengele cha ‘Best International Artist’ akichuana na Joe Young, Apollo na Escobar na Fil Straughan.

Wasanii waliowahi kushinda tuzo hizo ni pamoja MIMS, Nicky Minaj, Cory Gunz, J Cole, Freeway, Lil Mama, Killah Priest, Donny Goines, Esso, Stimuli, Torae, Serius Jones, Remy Ma, Styles P, Papoose, Saigon, Lumidee, Emilio Rojas, Fred The Godson na wengine.

Zoezi la kupiga kura limeanza jana August 10. Bonyeza hapa kumpigia kura Cindy Rulz.

Source: Bongo5

Author

Advertisement

 
Top