“Ningekuwa na uwezo wa kuwapiga wote ambao yaani wanaendelea huu mchezo uliopo, nafikiri ningewapiga na ningewafunga ningekuwa na amri hiyo.” Nay wa Mitego ameiambia Sunrise.
“Coz unajua kuna watu wanatengeneza hivi vitu, wanataka kuwatia watu stress. Wanataka watu ifike time waje wauane. Kuna beef tunaona zinakuwaga beef tu za kawaida. Lakini huu mchezo wa Ali Kiba na Diamond ni Mchezo ambao naona kama watu wanaoufanya uwe serious sana. Mimi sipendi nachukia.” Ameongeza rapper huyo wa ‘Itafahamika’.
Amewashauri Ali Kiba na Diamond kuachana kabisa na kinachoendelezwa kati yao na kuendelea na muziki kwa kuwa itafikia hatua mbaya ambayo wataumizana na kushindwa kufanya muziki.
Source: Times Fm