Mtalam III Mtalam III Author
Title: Diamond na Sheddy Clever wafanyiwa ‘ndivyo sivyo’ kwenye tuzo za AFRIMMA 2014
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Kumekuwa na sintofahamu kuhusu idadi ya tuzo alizozipata Diamond Platinumz kwenye tuzo za AFRIMMA kwa kuwa yeye na meneja wake walitangaz...
Kumekuwa na sintofahamu kuhusu idadi ya tuzo alizozipata Diamond Platinumz kwenye tuzo za AFRIMMA kwa kuwa yeye na meneja wake walitangaza kuwa wamepata tuzo zaidi ya moja huku mtandao maalum wa tuzo hizo ukionesha kuwa alipata tuzo moja tu.
Diamond baada ya kupokea Tuzo yake.

Baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo asubuhi, Diamond ameeleza utata uliotokea katika tuzo.

Amesema yeye alitajwa jukwaani kuwa mshindi wa tuzo mbili ya Msanii Bora wa kiume Afrika Mashariki na Wimbo Bora wa kushirikiana (My Number One Remix Feat. Davido), lakini baadae yalifanyika mabadiliko na tuzo hiyo kupewa Mafikizolo na wimbo wa Khona waliowashirikisha Uhuru.

Ameongeza kuwa hata Sheddy Clever pia alitajwa kuwa mshindi kama producer na kuoneshwa kabisa.

“Hata producer ambaye alikuwa ametangazwa ameshinda ni Sheddy Clever kwa sababu walimuonesha mpaka anapiga kinanda, maclip yake. Kama waliweza kuedit hata vinanda vyake anapiga yuko studio ina maanisha yeye ndiye alikuwa ameshinda.  Na wakatangaza collabo bora la kwangu mimi na Davido. Kwa sababu tuzo hii ndiyo tulienda kupewa kwenye stage kabisa pale. Lakini nyingine zilitangazwa kwenye TV.

“Lakini ghafla, mpaka kesho yake tukauliza mbona hatupewi tuzo zetu mpaka sasa hivi. Kwa sababu hata dada Jide naamini anaweza kupata leo au muda mfupi leo.  Sasa baadae wakaanza kusema kuna vitu vilikosewa sijui nini na nini…sikutaka tena kucomplain, kwa sababu nimeshapata yangu hii sikutaka kuleta matatizo mengine.” 

Hata hivyo, Diamond amesema anakubali kuwa alishinda tuzo moja na huenda kwenye kutangaza AFRIMMA walijichanganya wenyewe. Habari hii imeandikwa pia kwenye mtandao wa timesfm.co.tz.

Author

Advertisement

 
Top