Mtalam III Mtalam III Author
Title: Let’s Pray for Lulu: Ile kesi yake ya Mauaji bila kukusudia imefikia hapa
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambae anakabiliwa na kesi ya mauaji bila kukusudia ya mwigizaji Steven Kanumba  anatarajiwa kuanza kujib...
Mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambae anakabiliwa na kesi ya mauaji bila kukusudia ya mwigizaji Steven Kanumba  anatarajiwa kuanza kujibu mashitaka yake kwa mara ya kwanza Februari 17 2014 katika Mahakakama Kuu Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.
Msanii wa Bongo Movies, Lulu.

Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya kesi za mauaji ya bila kukusudia iliyotolewa na Mahakama Kuu kwa kanda ya Dar es salaam, kesi hiyo ya Lulu itasikilizwa mbele ya Jaji Rose huku ratiba ikionyesha kwamba mshtakiwa akishasomewa mashtaka na kujibu, Mahakama itapanga tarehe ya kusikiliza maelezo ya awali dhidi ya kesi hiyo.

Januari 29 mwaka 2013 Lulu aliachiwa kwa dhamana baada ya kesi hiyo kubadilishwa hati ya mashitaka kutoka kwenye kesi ya mauaji kwenda mauaji ya bila kukusudia ambapo badiliko hilo lilimpa nafasi ya kupata dhamana.

Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa Aprili 7 mwaka 2012 Sinza Vatican jijini Dar es Salaam, Lulu alimuua Kanumba bila kukusudia. Habari hii pia imeandikwa kwenye mtandao wa millardayo.com (source).



Tangazo | Click for more details:

• YS Shower Gels zinauzwa kwa bei nafuu (imported from Malaysia)
• Simu aina ya ‘Nokia N9’ Inauzwa kwa bei nafuu

Author

Advertisement

 
Top