Msanii wa filamu TZ, Lulu
Mbali na kukiri kuwa na uhusianano wa mapenzi, muigizaji huyo pia alikiri kuwa baada ya tukio hilo alitoka nje ya chumba walichokuwepo na kwenda kumwambia mdogo wake marehemu Kanumba, Setti Bosco kuwa Kanumba ametangulia mbele ya haki.
Akisoma hati ya mashitaka, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Monica Mbogo, alidai kuwa Aprili 7, mwaka 2012, Sinza Vatikani, Mkoa wa Dar es salaam, mshitakiwa alimuua bila kukusudia Stevin Kanumba.
Wakili Kombo, alidai kuwa pamoja na mambo mengine, marehemu Kanumba baada ya kufa, mwili wake ilipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo majibu yanaonyesha kwamba kifo chake kimesababishwa na uvimbe ndani ya ubongo.
Upande wa serikali una mashahidi watano pamoja na vielelezo wakati upande wa utetezi pia unatarajia kuwa na mashahidi watano na vielelezo. Habari hii pia inapatikana kwenye timesfm.co.tz na globalpublishers.info (Sources).