Keezywear Editor Keezywear Editor Author
Title: Vipi hii ikiletwa TZ: Wavaaji wa nguo za nusu uchi aka ‘vimini’ Uganda kufungwa mpaka miaka 10 jela
Author: Keezywear Editor
Rating 5 of 5 Des:
Taarifa ikufikie kwamba imepigwa marufuku kwa jinsia ya kike kuvaa nguo fupi (vimini) nchini Uganda na tayari Rais wa nchi hiyo Yoweri Musev...
Taarifa ikufikie kwamba imepigwa marufuku kwa jinsia ya kike kuvaa nguo fupi (vimini) nchini Uganda na tayari Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni amesaini rasmi sheria hii.

Japokuwa baadhi ya Wabunge walipinga kwamba marufuku hii inaingilia uhuru wa mtu kuvaa, wabunge wengi wameunga mkono uamuzi huo.

Unaambiwa marufuku hii ambayo imelenga kuepusha vitendo vya ubakaji na ngono zembe kutokana na ushawishi unaotokana na uvaaji huu, inahusisha pia nguo nyingine fupi ambazo zinaacha sehemu kubwa ya mwili wazi kama vile kifuani.

Mwanawake/Wasichana wataruhusiwa kuvaa mavazi mafupi kwenye matukio maalum tu yanayohusisha uvaaji huu kama vile michezo ambapo Waziri husika alifafanua. 

Sheria hii pia inawabana Wanamuziki wa kike ambao wamekua wakivaa nguo fupi kwenye show zao pamoja na video ambapo Waziri Lokodo amesema ‘hatutaki uhusike kufanya watu wakutamani au watamani kufanya ngono, hatutaki ushawishi chochote kwa jinsia ya kiume, kuwa na tabia njema kwa kuvaa kiheshima’

Vilevile vyombo vya habari yakiwemo Magazeti na TV, vimepigwa marufuku kuonyesha picha za watu wakipigana busu au picha zozote za Wanawake wakiwa nusu uchi.

Unaambiwa ukiukwaji wa sheria hii unaweza kusababisha kifungo cha miaka 10 hadi 15 jela. Habari hii imeandikwa pia kwenye millardayo.com na Bongo5.com.

Author

Advertisement

 
Top