Mtalam III Mtalam III Author
Title: Hermy B afunguka kuhusu ilipofikia ‘Bifu’ kati yake na AY na Mwana FA
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Moja kati ya habari nzuri ambazo zimewasurprise watu wengi leo ni kuhusu kurudi kwa urafiki uliokuwa umevunjika kati ya Hermy B, AY na mwana...
Moja kati ya habari nzuri ambazo zimewasurprise watu wengi leo ni kuhusu kurudi kwa urafiki uliokuwa umevunjika kati ya Hermy B, AY na mwana FA. AY na FA wamempa kampani kubwa producer Hermy B kwenye birthday party yake iliyofanyika usiku wa kuamkia leo na kupost picha kwenye mitandao ya kijamii.
Tovuti ya Times Fm imefanya mahojiano na Hermy B ambaye tayari ameingia nchini Kenya kwa ajili ya kuendelea na majukumu yake ya ujaji kwenye shindano Tusker Project Fame huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa jana (November 29).

Akiongelea kuhusu uhusiano uliopo kati yake na maswahiba wawili kwenye muziki AY na FA ambao awali walitofautiana kikazi na kila mmoja kuendelea kivyake, Hermy B amesema yeye na wasanii hao walimaliza tofauti zao siku nyingi na wamekuwa wakiishi kama washkaji kwa muda mrefu japokuwa hawakuweka kwenye media.

“By the way mimi na AY na Mwana FA unajua tunakutana mara nyingi sana, yaani tunapokutana ni nje ya nyumbani kwangu ambapo utanikuta niko mimi, AY, Mwana FA, yupo Fid Q,  Salama unamkuta yuko pale. So, most of the time tuko pamoja, hii ni kitu tu tumewaonesha kwamba as much as watu walikuwa wanafikiria labda kuna kitu kinaendelea lakini hapana, sisi tuko peace long time tumeamua ku-reveal tu sasa hivi,” Hermy B ameiambia tovuti ya Times Fm.

“Kiukweli sisi ni washikaji ambao tuko tight sana, nafikiri jamii tu ndio inaelewa kivingine. Unajua watu wengi wanafikiri mkishindwa kuelewana kitu fulani basi hamuwezi kuelewana, hapana…kwa sababu imagine sisi kila siku jioni kabla sijaingia kwenye nyumba yangu kulala nakutana na AY tunakaa tunapiga story mpaka saa nane za usiku ndo kila mtu anaenda kwake kulala,” amefunguka Hermy B.

Amesema hivi karibuni alikuwa na AY Nairobi, na walikaa na Fid Q na Prezzo na kupiga story usiku wote hadi asubuhi.

Hermy ambaye ni producer na C.E.O wa B’Hits amezungumzia mpango wao wa kufanya kazi tena kama ilivyokuwa zamani.

“Kazi tutafanya, unajua hizi ni plans za mbeleni na tumekuwa tunaongea ni jinsi gani tunaweza tukafanya kazi vizuri na kwa faida zaidi na kila mtu awe na furaha moyoni mwake unajua. Kwa hiyo kazi zitakuja hatuwezi kuwaambia lini, kesho kutwa au mwezi ujao.”

Ladha ya ngoma kali zitakazopikwa tena kama ‘Habari Ndio Hiyo’ itawakusanya tena mashabiki wa B’Hits, AY na FA pamoja kwa ajili kuusapoti muziki mzuri. Lini hasa?

Ameeleza Hermy B, “time ikifika, the right time statement itatoka kwamba tunafanya nini pamoja au nini kinaendelea interm of kazi and then wale mashabiki wote ambao walikuwa wanatupenda watatujoin watuongezee nguvu sasa tuweze kuifikisha Tanzania ambapo inatakiwa ifike.”

Kwa undani zaidi wa habari hii sikiliza ‘The Jump Off’ ya 100.5 Times fm leo kuanzia saa mbili kamili. Unaweza kusikiliza kupitia tovuti hii, bofya sehemu iliyoandikwa ‘Listen’ hapo juu.

Source: Times Fm Blog


Matangazo | Click them for more details:

• Tablet aina ya ‘Swag Tab - Expert 102’ Inauzwa kwa bei nafuu
• Simu aina ya ‘Nokia N9’ Inauzwa kwa bei nafuu

Like Keezywear on Facebook!

Author

Advertisement

 
Top