Baada ya ngoma yake ya ‘Kabinti Special’ kufungiwa kwa maana ya kuzuiwa kuchezwa kwenye vituo vya televisheni, kutokana na kutokuwa na maadili ya Kitanzania, Dully Sykes amesema amekata tamaa ya kuwa msanii wa Kimataifa kutokanana kitendo hicho kumvunja moyo.
Msanii wa Bongo flava, Dully Sykes
Akiongea kupitia XXL ya Clouds Fm, msanii huyo alianika hisia zake, namna alivyoumizwa na uamuzi huo huku akitoa mifano mbalimbali kama ‘kutoa video ikiwa na wasichana wamevaa majuba’.
Msanii huyo amesema serikali kupitia mamlaka ya mawasiliano TCRA imevipiga marufuku vituo vya televisheni visiipige video hiyo kutokana na mvunjiko wa maadili. Kwanza, maandishi yaliyopo kwenye t-shirt aliyovaa msanii Diamond, ‘Fuck the Police’ . Pili, ile swimming costume aliyovaa video queen.
Diamond Platnumz
Dully Sykes na Video Queen
Video nyingine zilizopigwa stop ni pamoja na ‘Uzuri Wako’ ya Jux, na ‘Nimevurugwa’ ya Snura.