Mtalam III Mtalam III Author
Title: Diamond aonesha picha ya ‘swimming pool’ linalojengwa kwenye nyumba yake mpya
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Ni staa ambae kila jicho la habari limekua likimuangalia kila wakati, kila anachofanya hata kama ni cha kawaida kimekua ni stori na kinapat...
Ni staa ambae kila jicho la habari limekua likimuangalia kila wakati, kila anachofanya hata kama ni cha kawaida kimekua ni stori na kinapata wepesi kuwafikia Watanzania bila yeye kuweka nguvu nyingi.
Pamoja na kwamba amekua kwenye headlines, Diamond amekua akisifika pia kwa kuthamini Watanzania wenzake na kuwapa ajira kupitia mgongo wake, amekua na timu anayozunguka nayo kila anapokwenda kwenye matukio yake lakini pia ameonyesha uzalendo zaidi kwenye ujenzi wa nyumba yake kwa kuwapa shavu la ujenzi Watanzania wenzake.

Huenda 2014 ukawa mwaka ambao mashabiki wake watashuhudia kumalizika kwa nyumba yake ambayo ni miongoni mwa maendeleo yake yaliyobadilisha fikra za vijana wengi wa Kitanzania kwamba muziki unalipa bigtime.

Hapa chini ni picha ya swimming pool a.k.a bwawa la kuogelea analolijenga nyumbani kwake ambalo baada ya kuweka hii picha, ameiambatanisha na maneno haya:

Wachina wa nini wakati Watanzania wenzangu wanaweza pia???... #SwimmingPool #MyNewHome can't wait
Source: Millard Ayo

Author

Advertisement

 
Top