Katika pitapita yangu kwenye mitandao ya kijamii nikakutana na ujumbe huu ambao unaonesha utofauti kati ya wasanii wakubwa, Ali Kiba na Diamond. Mwandishi wa habari hii amejaribu kuelezea jinsi Diamond anavyozitumia fursa anazozipata vizuri na jinsi Ali Kiba anavyozipuuza. Soma hii kitu (hapo chini) halafu niambie, Mwandishi yuko sahihi?
“Hata kama sio shabiki wa diamond ila kuna kitu lazima uwe kinakuvutia kutoka kwake.Unaweza kujitahidi kumchukia labda kutokana na skendo zake za nje ya muziki wake ila ukirudi kwenye muziki wake nadhani anastahili kuwa pale alipo. Kuanzia muonekano wake mpaka anavyoweza kujibrand kimataifa na anavyojua kucheza na akili za mashabiki.
Wasanii wengi wa bongo flava wana tabia ya kuridhika kwa mafanikio yao ila Diamond toka atoke na Kamwambie mwaka 2009 mpaka 2013 amezidi kwenda juu bila kuonyesha kusuasua wala kutetereka.
Angalia video ya Number 1. Wimbo unaweza sema ni wa kawaida kabisa ukilinganisha na Mbagala, Kamwambie au Nitarejea, ila akili ya kwenda kufanya video Cape Town, South Africa kumeufanya wimbo uwe Number 1 kama jina lake lilivyo.
Ushawahi kujiuliza Ali Kiba yupo wapi pamoja na kuwa kila mtu anajua ni mkali kuliko Diamond? Ali Kiba toka atoe My Everything mwisho wa mwaka jana amepotea hata video ajatoa.Tukaja kumuona kwenye Kidela na Abdu kiba bila kurefusha maneno Ali anashindwa kuufanya muziki wake kama mashabiki wake wanavyotarajia labda pengine angekuwa anafukuzana na Diamond ila matokeo yake vijana wake kama Rich Mavoko na Dimpoz ndio wapo nyuma ya Diamond huku Ali akibaki msanii mkali ambae ameshindwa kuendelea kutuonyesha ukali wake sijui anawaza nini!
Ushawahi kujiuliza kama ule wimbo wa Airtel Hands Across the World waliopiga wakina R Kelly, Fally Ipupa, 2face na wengine, kama nafasi ile angeipata Diamond leo angekuwa wapi? Diamond leo anatuletea Number 1 Remix ft Davido kila mtu anaisubiri kwa hamu ila Ali alishindwa hata kutuletea Remix ya Dushelele ft Fally Ipupa pamoja kukaa nae wiki nzima wakifanya wimbo pamoja.
Diamond ni mjanja anayejua biashara ya muziki ilivyo labda pengine ni Management yake inayomsimamia. Diamond kaweza kuubadili muziki wetu kwa kiasi chake leo ndio msanii anaelipwa pesa nyingi kwa show. Nampenda ali kiba,naipenda sauti yake,anajua muziki kuliko Diamond ila Ali ameshindwa kubadilika na kukubali soko la muziki linataka nini.
Amka Ali huyu Diamond hakuwezi ila usipokuwa makini utajikuta nyuma ya Rich, Barnaba, Dimpoz na Ben Pol maana muziki sio kuimba peke yake, muziki ni biashara pia.”
Okay, sasa niambie maoni yako, unaonaje kuhusu hili?
Like Keezywear on Facebook!