Msanii wa Bongo flava, Ray C
“Badilika babaa. Nakuombea sana ujitambue na ubadili mwendo wa Maisha yako. Wewe bado ni kijana mdogo sana na una kipaji cha pekee. Kila Mtu Ana changamoto yake ya maisha,angalia wapi ulipokosea, litambue tatizo halafu kubali kwamba una tatizo then rekebisha Hilo tatizo. Anza Maisha mapya, Badilika.
Majanga yote yanayokukuta ni ishara tosha kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwamba unakoelekea siko, Kama una akili timamu basi utagundua Hilo na utajirekebisha babaa, Nakuombea kila la kheri katika mabadiliko ya Maisha yako. Karibu Kwenye Tiba ya Methadone. Methadone Kiboko ya Madawa.” aliandika Ray C.