Keezywear Editor Keezywear Editor Author
Title: Weusi wampiga ‘stop’ Lord Eyez, chanzo ni tukio hili
Author: Keezywear Editor
Rating 5 of 5 Des:
Msemaji wa kundi la Weusi, Nikki wa Pili amefunguka kuwa rapper Lord Eyez amesimishwa kazi katika kampuni hiyo na kwamba kwa sasa sio ‘membe...
Msemaji wa kundi la Weusi, Nikki wa Pili amefunguka kuwa rapper Lord Eyez amesimishwa kazi katika kampuni hiyo na kwamba kwa sasa sio ‘member’ wa kundi hilo.
Wasanii wanaounda kundi la Weusi

 “Kitu ambacho naweza kusema kutoka Weusi ni kwamba Lord Eyez tumemsimamisha kazi kikampuni.” Amesema Nikki wa Pili na kusisitiza kuwa hajafukuzwa kazi bali amesimamishwa.

Hata hivyo, Nikki wa Pili hakuwa tayari kuweka wazi moja kwa moja sababu zilizopelekea Weusi kumsimamisha kazi rapper huyo.

“Hizo ni confidential, ni issue za kampuni hatuwezi kuziweka wazi lakini Lord Eyez tumemsimamisha kazi hiyo ndio taarifa ambayo tunaitoa kwa media.” Nikki wa Pili ameeleza.

Ameongeza kuwa kwa sasa matukio yote yanayotokea kwa upande wa Lord Eyez yatakuwa yanamhusu yeye binafsi na hayatakuwa na uhusiano wowote na kampuni.

Hii inamaanisha hivi sasa Weusi inaundwa na Joh Makini, Nikki wa Pili, G-Nako na Bonta.

Uamuzi huo wa Weusi umekuja wakati ambapo kumekuwa na taarifa kuwa Lord Eyez alikamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za wizi Jumamosi, huko Arusha na baadhi ya picha za tukio hilo kuonekana. Taarifa hizo zimedai kuwa anatuhumiwa kwa wizi wa laptop aina ya 'Dell'.

Mwaka juzi, Lord Eyez alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa Power Window za gari la Ommy Dimpoz, lakini Ommy alitangaza kumsamehe msanii huyo.

Weusi walichukua dhamana ya kumtetea na kumuwekea mwanasheria huku wakifanya mikutano na waandishi wa habari ili kuitengeneza image ya kampuni hiyo ambayo ilikuwa imewekewa alama na tuhuma za Lord Eyez ambaye ni member wa kundi la Nako 2 Nako.

Kufuatia uamuzi wa Weusi, G-Nako ameeleza mtazamo wake pia kwa kuzingatia kuwa yule ni mwanafamilia mwenzake wa kundi hilo.

“Nafikiri alichokwambia Nikki ni kitu ambacho tumekubaliana watu wote na msimamo kama wa kampuni ndio huo.” Amesema G-Nako. “Haijalishi kama ni member, ni Nako 2 Nako ni nini lakini Lord Eyez ni mmoja wa wanahisa wa Weusi na kilichofanyika ni hicho na maamuzi ndio hayo, hilo swala liko ndani ya Kampuni.”

Baada ya Lord Eyez kusimamishwa kazi, hivi sasa Nako 2 Nako ina mwanahisa mmoja tu kwenye kampuni ya Weusi, huku wana River Camp wakiwa watatu.  Biashara inaendelea na sheria inafuata mkondo.

Hata hivyo, bado kuna mkanganyiko kati ya tafsiri ya tamko la Weusi kwa baadhi ya watu, ambapo wengi wamechukulia ‘kusimamishwa’ kama ‘kufukuzwa’. Hii imempelea Joh Makini kufafanua.


“Lord Eyez hajafukuzwa wala kutengwa kama wengi mnavyoitafsiri.” Joh Makini ameandika Instagram na kupost picha akiwa na Lord Eyez. Habari hii imeandikwa pia kwenye timesfm.co.tz (source).

Author

Advertisement

 
Top