Mtalam III Mtalam III Author
Title: Unahisi Ray C yupo sahihi kumwombea Jackie Cliff afe!?
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Mambo vipi? Kabla ya yote niwatakie kheri ya mwaka mpya wa 2014. Sasa turudi kwenye Tujadili yetu ya leo maana mengi yamejiri. Wengi wetu t...
Mambo vipi? Kabla ya yote niwatakie kheri ya mwaka mpya wa 2014. Sasa turudi kwenye Tujadili yetu ya leo maana mengi yamejiri. Wengi wetu tunajua yaliyomkuta Jackie Cliff huko China. 
Mrembo huyo ambaye alianza kupata umaarufu baada ya kushiriki mashindano ya Miss Tanzania na kisha kutokea kwenye video ya She Got A Gwan ameshikiliwa Macau, China baada ya kukamatwa akiwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin.

Mzigo wa madawa hayo ulikuwa wa Kilo 1.1 ambao Jackie alikuwa ameubeba tumboni akiusafirisha kutoka Bongo akapita Kenya, Thailand na hatimaye akakamatwa nao China. Mtandao wa dailychina.com ulitaarifu kwamba mzigo huo unagharimu takriban shillingi mil. 223 za kitanzania.
Kiubinadamu tunatambua kwamba Jackie Cliff anatakiwa kuonewa huruma na tunajua kwamba ametumika tuu kusafirisha madawa hayo (yeye si mmiliki) ndo maana baadhi yetu tumekuwa tukiombea aachiwe japo itakuwa ngumu.

Tofauti na sisi, kuna watu wengine (watanzania) hawana huruma na mrembo huyo, wenyewe wanataka Jackie Cliff ahukumiwe ili watu wengine wajifunze kupitia yeye. Watu hawa wengi wao ni walioathirika na utumiaji wa madawa ya kulevya au wenye watu wa karibu ambao wameathirika, so sishangai mawazo yao kwasababu tabu walizopitia au wanazopitia ni kubwa!
Mmoja kati ya watu hao ni msanii mkongwe wa Bongo flava, Ray C. Kupitia akaunti yake ya Instagram, msanii huyo alifunguka hivi: 

“Wewe tulia mi nna hasira maana najua walichonifanya hawa wauzaji!?! niliingia kwenye madawa Na niliwapa kila Kitu Hawa wauzaji ili nipate unga maana tayari nilikuwa nimeshaathirika, hawakunionea huruma pamoja Na Aibu yote walichotaka wao ni pesa ili nipone ndio niheme!!!!!! nilipokuwa Na hela walinithamini ila nilipoishiwa walinilaza kwenye box Na arosto!!!

niliwaomba hata kidogo ili nisiumwe but hawakunielewa ingawa nilishawapa mamilioni ya hela Na nyumba nikauza!!!!!!! sikia tu arosto na omba isiwahi kutokea kwa ndugu yako wala mtoto wako!!!!!!jinsi mama yangu alivyohangaika na mimi k*manina huyu jacky afe tu mmbwa mkubwa!!!! na muuaji ndugu za watu wanalala barabarani mmpaka tunaimbwa teja wa mapenzi!!!!


yani acha kabisa!!! wafe wanyongwe, mafirauni wenye dhambi kubwa mbele ya mungu!!! ktk jina la yesu!!!! Wanyongwe!!!!!!! Kill them!!!!”


Kuna baadhi walimsupport na kuna wengine wamemponda kutokana na alichokiandika. Mie sina shida hapo kwasababu najua ana hasira na ameexpress feelings zake, and ana point!

Sasa Tujadili, unahisi Ray C yupo sahihi kumwombea Jackie Cliff afe??? 

Author

Advertisement

 
Top