Keezywear Editor Keezywear Editor Author
Title: Ex-Girlfriend wa JB, Selena Gomez ajinadi, ‘mimi sio mwanamke wa usiku mmoja’
Author: Keezywear Editor
Rating 5 of 5 Des:
Ex-Girlfriend wa Justin Bieber, Selena Gomez ambaye ni msanii wa filamu nchini Marekani amejinadi kuwa yeye ni mwanamke bora. Selena Gomez...
Ex-Girlfriend wa Justin Bieber, Selena Gomez ambaye ni msanii wa filamu nchini Marekani amejinadi kuwa yeye ni mwanamke bora. Selena Gomez mwenye miaka 19 tu alipitia kipindi kigumu kidogo wakati wa uhusiano wake wa kimapenzi na JB.
Staa huyo wa filamu ya Another Cinderella amefunguka katika interview na jarida la Vogue litakalotoka November 19, mwaka huu. Alifunguka kama ifuatavyo:

Siku zote nitakuwa mwanamke unayetaka kumpeleka nyumbani kwa wazazi wako na sio mwanamke wa usiku mmoja.” Alisema Selena.

Mwimbaji huyo ambae alishahangaika na mapenzi ya Justin Bieber aliitoa sentensi hiyo wakati ambapo anaelezea kuhusu kipindi kigumu katika mahusiano ya mapenzi hasa pale umpendae anapokuacha.

Aliongelea kuhusu hali ya kuwa katika kipindi kizuri na pia kuwa katika kipindi kigumu. Selena sio mwanamke wa kupotezea hisia zake.

Unaingia katika mapenzi na yanakumeza kabisa, sehemu ya moyo wako inakuwa imevunjika, na sehemu nyingine inakuwa na hisia za kukataa hali hiyo, sahau kuhusu hilo, naweza kufanya chochote nachotaka. 

Nimejaribu hivo lakini sikuwahi kuwa msichana wa aina hiyo. Siku zote ntakuwa mwanamke unaetaka kumpeleka nyumbani kwa wazazi wako, sio wa usiku mmoja.” Amesema Selena.

Author

Advertisement

 
Top