Mtalam III Mtalam III Author
Title: Diamond atua Nigeria kwa ajili ya kufanya video na wasanii hawa
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Diamond tayari ameshafika nchini Nigeria kwa ajili ya kazi ya kimuziki pamoja na wasanii nchini humo ambapo baada ya kufanya remix ya My Nu...
Diamond tayari ameshafika nchini Nigeria kwa ajili ya kazi ya kimuziki pamoja na wasanii nchini humo ambapo baada ya kufanya remix ya My Number One na Davido, kazi inaendelea na sasa amemfata huko huko kwao Nigeria.
Diamond anaelezea kwamba baada ya kufanya ngoma na Davido, pia ngoma nyingine amefanya na Iyanya japokuwa watu wengi hawafahamu kuhusu hiyo collabo.

Lengo lake kubwa lilikuwa si kufanya collabo tu bali anasema alitaka kujenga ukaribu na wasanii wa Nigeria ndiyo maana ameamua kwenda kufanya video hukohuko Nigeria.

Japokuwa hajasema ni production gani atatumia, hivi sasa Diamond ameshafika nchini Nigeria na atarudi baada ya kufanya video mbili ambapo moja akiwa na Davido na nyingine pamoja na Iyanya.


Matangazo | Click them for more details:

• Simu aina ya HTC Desire S ‘S510E’ inauzwa kwa bei nafuu
• Simu aina ya ‘Nokia N9’ Inauzwa kwa bei nafuu

Source: TZA

Like Keezywear on Facebook!

Author

Advertisement

 
Top