Keezywear Editor Keezywear Editor Author
Title: The Interview: Majibu ya Diamond kuhusu uchawi, ugomvi wake na AliKiba, collabo na Tuzo anazowania
Author: Keezywear Editor
Rating 5 of 5 Des:
Diamond Platnumz alikuwa live kwenye XXL ya Clouds FM , kuna vingi kaviongea exclusive, nilipata nafasi kumsikiliza na hivi ni baadhi ya v...
Diamond Platnumz alikuwa live kwenye XXL ya Clouds FM, kuna vingi kaviongea exclusive, nilipata nafasi kumsikiliza na hivi ni baadhi ya vitu alivyoviongelea jana June 6, 2015.


1. Unadhani Diamond anaamini uchawi?
 “Japokuwa vitabu vya dini vinasema ‘ndele’ zipo lakini  haupaswi kuamini… Kuamini ni sawa na kumkiuka Mwenyezi MUNGU”

2. Kuna beef kati yake na Ali Kiba? Na vipi zile Team kwenye Mitandao ya Kijamii?
“Sijawahi kuwa na beef nae hata siku moja… Sioni kama kuna ubaya wowote, kila mtu ana maamuzi kumchagua mtu anayemtaka yeye kumshabikia, huwezi kumlazimisha mtu. Wawachukue msanii fulani na msanii fulani wawashindanishe na wasanii wa nje, ukiwashindanisha wasanii wa Tanzania haiwezi kusaidia Industry yetu.”

3. Kuna malipo ya collabo?
“Sijawahi kufanya malipo kufanya nyimbo na mtu yoyote.. Mwanzoni ilikuwa tabu, sasahivi wanafahamu kwamba kufanya nyimbo na Diamond inakuwa rahisi nyimbo kufahamika East Africa... nimefanya collabo na karibuni wasanii wote wakubwa Africa.”

4. Show ya MTV Road to MAMA Nigeria aliipataje?
“Ni mwaliko wa MTV, wa kwanza nilipewa South Africa nikafanya vizuri, wakaona wanipe na sehemu nyingine”


5. Hiki ndio alichojibu kuhusu kupigiwa kura za MTV Awards 2015!
“Wanaoona kuna umuhimu hizi Tuzo zije Tanzania waendelee kupiga kura, anayeona ni sawa kumpigia mwingine ni sawa… Uzalendo haununuliwi, huwezi kumlazimisha mtu. Muziki wetu umekuwa na nafasi nzuri sana Africa, ni kazi kubwa sana imefanywa. Kuna utaratibu unaandaliwa kuona kama tutaweza kuwabeba watu kama mashabiki na Watangazaji. Tupige kura kwa siku hata mara moja sio mbaya, kama tulichukua ‘Channel O’ sasa hivi tutashindwaje”

Source: Millardayo

Author

Advertisement

 
Top