
Nay amesema kuwa hadi sasa tayari amekamilisha collabo mbili na wasanii wa kimataifa, ikiwemo aliyofanya na msanii wa Nigeria, RunTown ambayo production yake imefanywa na Uhuru wa Afrika Kusini.
Video ya collabo hiyo ambayo itafanyika hivi karibuni ataifanya pia nje ya Tanzania.
“Nimeshafanya ngoma na wasanii ambao ni International tayari nyimbo kama mbili hivi, nimefanya na RunTown tayari tumeshamaliza na ngoma imeisha ni production ya Uhuru, so tumefanya kila kitu cha nje, tunatarajia kushoot video hivi karibuni.” Alisema Nay Wa Mitego kupitia Friday Night Live ya EATV.
Kuhusu video ya collabo yake na Diamond ‘Mapenzi au Pesa’, Nay amesema wanatarajia kushoot hapa hapa Tanzania wiki Ijayo Diamond atakapokuwa amerejea.