Keezywear Editor Keezywear Editor Author
Title: Dudubaya ahoji: Muziki wa Tanzania unapenya vipi wakati unawakilishwa na msanii mmoja tu?
Author: Keezywear Editor
Rating 5 of 5 Des:
Dudu Baya anapingana na kauli kuwa muziki wa Tanzania umepenya Afrika. Akiongea kwenye kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV, rapper ...

Dudu Baya anapingana na kauli kuwa muziki wa Tanzania umepenya Afrika. Akiongea kwenye kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV, rapper huyo amesema muziki wa Tanzania haujapenya kwakuwa anayeiwakilisha Tanzania ni mmoja tu, Diamond.

Amesema ili muziki wa Tanzania uweze kusemwa umepenya kimataifa ni lazima kuwepo na wasanii wengi wanaofanya vizuri kama ukubwa wa Diamond kwa sasa.

Amedai kuwa muziki wa Nigeria ndio uliopenya zaidi kwakuwa kuna wasanii wengi wanaofanya vizuri na wenye ukubwa sawa tofauti na Tanzania.

Rapper huyo amezitaja chuki, wivu na kubaniana ndio sababu kubwa za muziki wa Tanzania kushindwa kupenya.

Copied from here!

Author

Advertisement

 
Top