
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Breezy na mama wa mtoto huyo, Nia Guzman wamekuwa wakipishana kuhusiana na mahitaji ya mtoto huyo hivyo anamtaka jaji amtambue kama baba halali wa mtoto huyo, hatua ambayo itampa haki ya kupambana na Nia juu ya mtoto huyo.
Chris anadaiwa kumlipa Nia kile anachoamini ni kiasi sahihi kwa mwezi ambacho ni dola 2,500 kwa mwezi japo anataka apewe $15,000 kwa mwezi ili kumtunza mtoto.
Copied from here!