Mtalam III Mtalam III Author
Title: Sakata la kuurudia Unga: Ray C asema ‘Kama mnataka kuniua nichomeni hata kisu...’
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Wote tunafahamu kwamba msanii wa Bongoflava,  Ray C aka  ‘ Kiuno bila mfupa ’  alikuwa kwenye wakati mgumu sana wakati alipojihusisha na m...
Wote tunafahamu kwamba msanii wa Bongoflava, Ray C aka Kiuno bila mfupa alikuwa kwenye wakati mgumu sana wakati alipojihusisha na madawa ya kulevya kiasi kwamba Rais J.K aliingilia kati kumtoa kwenye alosto na kuokoa maisha ya msanii huyo.

Sasa Gazeti moja limeandika habari kwamba msanii huyo amerudia Madawa ya Kulevya kitu ambacho kimemtia hasira sana. Ray C amlipost picha ya gazeti hilo ambalo liliandika Daktari: JK muokoe Ray C! kwenye akaunti yake ya Instagram na kusema maneno haya mazito.

“MLISEMA NITAKUFA BAADA YA SIKU 190 HAYA HATA BADO SIKU HAIJAFIKA MNAANDIKA TENA HUU UPUUZI, HIVI NYIE MNATAKA KUNIULIA MAMA YANGU JAMANI? HAYA SASA MAMA YANGU PRESHA JUU USO WOTE UMEMVIMBA SABABU YA PRESHA KISA HILI GAZETI LENU! 

MBONA HAMNIONEI HURUMA MWENZENU BADO HATA SIJAMALIZA MATIBABU MNAANZA KUNIOMBEA MABAYA! KAMA MNATAKA KUNIUA NITAFUTENI MNICHOME HATA KISU NIFIE MBALI LAKINI SI MAMA YANGU!! NAANDIKA HII MESEJI CHOZI LINANITOKA! 


NAWAOMBA MSINIULIE MAMA YANGU KWA PRESHA NA HIZI HABARI ZENU... MSINIOMBEE MABAYA MWENZENU NIMEPITIA KWENYE MTIHANI MGUMU SANA KWENYE MAISHA YANGU, KAMWE SITORUDI NYUMA, NAOMBA SAPOTI YENU... MSINIOMBEE MABAYA...”

Author

Advertisement

 
Top