Mtalam III Mtalam III Author
Title: Msanii wa Bongo Movie, Slim apandishwa kizimbani kwa madai haya
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa Bongo Movie ambaye anajulikana kwa jina maarufu la Slim amepandishwa kizimbani wiki ilopita. Kwa mujibu wa mtandao wa Bongomo...
Msanii wa Bongo Movie ambaye anajulikana kwa jina maarufu la Slim amepandishwa kizimbani wiki ilopita.

Kwa mujibu wa mtandao wa Bongomovie, Msanii huyo alipandishwa kizimbani katika mahakama ya Mwanzo, Magomeni. Mtandao huo uliandika hivi:

Mwigizaj wa filamu hapa nchini, Salim Omary ‘Slim’ amedaiwa kupandishwa mahakamani baada ya mkewe, Asia kudai talaka. Chanzo makini kilisema kwamba, Slim alipandishwa kizimbani Jumatatu wiki iliyopita katika Mahakama ya Mwanzo-Magomeni jijini Dar kwa madai ya talaka. 

 Baada ya kuzipata habari hizo gazeti hili lilimtafuta Slim ambapo alikuwa na haya ya kusema: 
“Ni kweli nimepelekwa mahakamani na kesi itatajwa tena Januari 28, mwaka huu na madai yaliyonipeleka ni aliyekuwa mke wangu anahitaji talaka, ukweli inaniuma sana lakini basi namwachia Mungu.”

Source: GPL & Bongomovie.

Author

Advertisement

 
Top