![]() |
Diamond na Zari |
Sasa kwa mujibu wa mtandao wa Bongo5, nikaona taarifa kwamba Diamond anatarajia kuitwa baba baada ya kupost picha ya Ultrasound kwenye akaunti yake ya Instagram. Na swali ni kwamba je anatarajia kupata mtoto huyo kweli? Na atazaa na nani? Zari au mwingine?. Mtandao huo uliandika hivi:
![]() |
Post ya Diamond kwenye Instagram |
“Uhusiano wa Diamond Platnumz na Zarinah Tlale a.k.a Zari The Boss Lady sasa unaelekea kwenye level nyingine. Diamond ameweka wazi kuwa anatarajia kuwa baba. Kupitia Instagram Diamond alipost picha ya ‘ultrasound’ inayoonesha kiumbe kilichoko tumboni mwa mama na kuandika:
“I can not wait to have you on my hand”. Hata hivyo aliifuta post hiyo baada ya dakika mbili. Kwa picha na maneno hayo, Platnumz amethibitisha kuwa yeye na Zari wanatarajia kupata mtoto.
Zari tayari ni mama wa watoto watatu wa kiume aliowapata kwenye uhusiano wake uliopita.”
Source: Bongo5.