Kila ijumaa naandaa au kushare Makala/Interviews katika mtandao huu. Dhumuni ni kujifunza kupitia Makala ambazo zinaelemisha na kuburudisha na pia kujua mambo mbalimbali kupitia Interviews wanazofanyiwa watu maarufu.
Wiki iliyopita kulikuwa na bonge la B'day Party ya Diamond Platnumz. Shughuli hiyo ilihudhuriwa na watu wengi maarufu waliopata mualiko maalum, mmoja wa wahudhuliaji alikuwa mtangazaji maarufu wa Clouds Fm, B12 aka BDozen.
B12 alifanyiwa interview ndogo na Bongo5 na alifunguka vitu vichache kuhusu mafanikio ya Diamond, soma hapa alichokisema:
Anaonaje ukuaji wa Diamond kimuziki?
B12: Diamond nimekutana naye mwaka 2009 kwenye show ya Fiesta iliyofanyika Viwanja vya Posta, show ambayo Busta Rhymes naye aliperform. Show aliyopiga pale ilionesha jinsi gani ana njaa kwasababu hata wasanii wengine wakubwa waliokuja kuperform baada yake walikuwa wanaizungumzia show ya Diamond.
So ni msanii mwenye njaa, haridhiki na alinachokipata, sio kwamba ni kidogo no, anaamini anaweza kupata zaidi kwa kufanya kazi nzuri. Ndo hicho nachokiona kwa Diamond.
Anazungumziaje kuhusu kutajwa (kuwa nominated) kwa Diamond kwenye Tuzo mbalimbali Afrika na nje ya Afrika?
B12: Hii ni ishara kwamba ni msanii anayekubalika na kila mtu anamuona mbali, kwasababu kila categories ambazo anatajwa zile za 'Msanii mpya' au msanii ambaye anaonekana anakua. So kwangu mimi naona its time, anadeserve kwasababu anafanya kitu kizuri.
Kitu gani anahisi wasanii wakubwa na hawa wanaokuja ambao hawajafika alipofika Diamond wanaweza wakajifunza kutoka kwake?
B12: Aaah kuna neno moja la mtaani linasema kwamba 'ana njaa', sio kwamba ana njaa (hajashiba) ila ana njaa ya mafanikio. Nafikiri kila mmoja akionesha njaa yake ya hali ya juu kwamba kuna sehemu flani nataka nifike na bado sijafika na kutodharau kule ambapo umetoka ndicho kinachomfanya Diamond aendee kufanikiwa.
Yaani hata unapozungumza nae anaonekana anaheshimu anachokifanya, anaheshimu wale wanaomsupport, anaamini kwamba pale alipofika amefika kwa sababu ya watu flani flani na flani kwahiyo hawa nikiendelea kuwa nao pamoja nitaweza kufika mbali zaidi, tofauti na wasanii wakubwa, nafikiri hicho ndo kinawafelisha wengi.
Lakini kama kila mmoja angekuwa anamuheshimu kila mmoja kwa nafasi yake ambayo yupo, i'm sure leo kila mmoja angekuwa anafurahia mafanikio ya kila msanii mkubwa kuliko vile Diamond anavyofanya.
Endelea kufatilia Keezywear.com kwa ajili ya Interviews zingine kila siku ya Ijumaa.
B12 (Kushoto), Diamond, Joh Makini na Romy (Kulia)