Keezywear Editor Keezywear Editor Author
Title: U Shud Kno: Smartphones zinaua matumizi ya vifaa vifuatavyo
Author: Keezywear Editor
Rating 5 of 5 Des:
Habari za Jumatatu? Kama ilivyo kawaida, kila siku kama ya leo nakupa nafasi ya kuweza kujua mambo mbalimbali. Segment hii inaitwa ‘ Acha Ni...
Habari za Jumatatu? Kama ilivyo kawaida, kila siku kama ya leo nakupa nafasi ya kuweza kujua mambo mbalimbali. Segment hii inaitwa ‘Acha Nikujuze’, ipo kwa lengo la kufahamishana zaidi kuhusu mambo ambayo hujafikiria kuyawaza kwa undani au yatakayokushangaza zaidi.


Kama wewe ni mtumiaji wa Smartphones utagundua kwamba simu hizo zina uwezo wa kufanya kazi za vitu vingi sana kwa wakati mmoja. So kuna vitu vingi havitumiki kihivyo siku hizi kwa sababu ya uwepo wa Smartphones. Kama ulikuwa hujui, acha nikujuze kuhusu vitu 9 ambavyo vinakufa kwasababu ya uwepo Smartphones hapa:


 #1 – Cameras



Siku hizi cameras hazina jipya zaidi ya kutumiwa na Professional Photographers. Smartphones zinapiga picha nzuri kama au zaidi ya camera ambazo tulikuwaga tunabeba zamani. Pia ni rahisi sana kushare picha zako kwenye facebook, instagram, email au twitter (you only need few clicks) kuliko kama ungepiga kwa kutumia camera ya kawaida.

#2 – Mp3 Players
Hivi kuna mtu anahitaji kuwa na MP3 Player siku hizi? Smartphones zina music-listening apps za kutosha, so MP3 Players zinaonekana ni kitu ambacho kimepitwa sana.

#3 – Basic Calculators
Kuna umuhimu gani wa kuwa na calculator wakati kila simu siku hizi inayo? na wale ambao wanahitaji kukokotoa mahesabu zaidi ya kuzidisha na kugawanya zipo applications nyingi tu za scientific calculator ambazo unaweza ukadownload kwenye Smartphones na kutumia.

#4 – Alarm Clocks
Kwa kifupi, alarm clocks hazina jipya siku hizi, hata saa za kawaida. Kama unabisha ukikutana na mtu muulize sasa hivi saa ngapi uone kama hajatoa simu na kutazama saa. Kwanza smartphone inakupa option ya kuchagua wimbo ambao utakuwa unatumika kukuamshia, halafu unalala nayo karibu, kwanini usiitumie kama kifaa cha kukuamshia?

#5 – Maps & GPS Sat Navs
Leo, smartphones zinakuwa na Navigation System na Google Maps zake zenyewe. Navigation system inatumika kukuongoza na kukufikisha sehemu unayotaka kwenda kwa kufatisha ramani ya sehemu husika.

#6 – Landline Phones & Payphones
Kwanini ujisumbue kupiga au kupigiwa simu kwenye Landline phone au Payphone wakati njia rahisi ya kumpata mtu ni kupitia simu yake ya mkononi  (eg smartphone) ambayo anaenda nayo popote?

#7 – Letter Writing
Hahaa, siku hizi kuna njia kibao za kuwasiliana kwa maandishi. Nani anataka kuandika barua halafu asubiri kitambo kidogo itumwe, ifike na ijibiwe wakati unaweza ukaandika email au text kupitia smartphone yako na ukatuma na ikajibiwa ndani ya dakika chache?

#8 – Paper Diaries
Hakuna haja ya kuwa na Diaries wakati smartphones zina kila kitu, mpaka alarm remainders kwa ajili ya appointments.

#9 – Handheld Games Consoles
Modern Smartphones zina screen sizes, processing power, memory na storage capacity, ambayo inaziwezesha simu hizo kuweka hata games zenye uwezo mkubwa.

Kiukweli smartphone imeua vitu vingi zaidi vya Teknolojia kuliko kifaa kingine chochote. Toa maoni yako kuhusu Acha Nikujuze ya leo na share na wengine. Endelea kupitia keezywear.com kila siku.

Author

Advertisement

 
Top