Keezywear Editor Keezywear Editor Author
Title: The Lists: Wasanii 15 wa HipHop duniani walioingiza fedha nyingi zaidi kwa mwaka 2014
Author: Keezywear Editor
Rating 5 of 5 Des:
Mambo niaje Jumanne ya leo? Kila siku kama ya leo kwenye mtandao huu wa kijanja kunakuwa na ‘ The Lists ’. Segment hii inakupa nafasi ya kuw...
Mambo niaje Jumanne ya leo? Kila siku kama ya leo kwenye mtandao huu wa kijanja kunakuwa na ‘The Lists’. Segment hii inakupa nafasi ya kuweza kujua orodha ya issues mbalimbali duniani, itakupa hamu ya kutaka kujua issue/mtu yupi yupo juu katika orodha husika.


Leo kwenye kipengele hiki nakupa orodha ya wasanii 15 wa Hiphop duniani walioingiza mkwanja mrefu zaidi kwa mwaka 2014. List hii ni kwa mujibu wa Forbes. Here is the list:

1. Dr Dre:
Kwa hivi sasa Dre amewatupa mbali wasanii kibao juu ya mafanikio ya kifedha ambapo ndani ya miezi 12 iliyopita ameingiza dola milioni 620 (bila makato). Kiwango hicho cha fedha sio tu kuwa ni kiwango kikubwa sana kuingiza ndani ya mwaka kwa msanii (kilichowahi kuripotiwa na Forbes) bali ni zaidi ya kuchanganya mapato ya wasanii 24 wanaomfata nyuma katika list ya wasanii wa hiphop wenye mkwanja 2014.

2. Diddy:
3. Jay Z:

Diddy na Jay Z ambao wamefungana, wote wakiwa wameingiza dola milioni 60, kama unakumbuka diddy alikuwa nafasi ya kwanza mwaka jana na Dre alikuwa nafasi ya tatu.

4. Drake:
Drake ambaye ameingiza dola milioni 33, yakiwa ni mapato kutokana na album yake ya nne Nothing Was the Same, ambayo imeuza kama copy millioni 4 duniani kote huku mkwanja mwingine ukiwa umetokana na tour ya Arena na endorsement deal ya Nike “Jordan” zimempeleka kuongeza kipato mara tata ya mwaka jana alipokuwa na kipato cha dola milioni 10.5

Wengine katika list hiyo ni pamoja na:

5. Macklemore & Ryan Lewis: $32 million.
6. Kanye West: $30 million
7. Birdman: $24 million
8. Lil Wayne: $23 million
9. Pharrell Williams: $22 million
10. Eminem: $18 million
11. Nicki Minaj: $14 million
12. Wiz Khalifa: $13 million
13. Pitbull: $12 million
14. Snoop Dogg: $10 million
15. Kendrick Lamar: $9 million

Author

Advertisement

 
Top