Mtalam III Mtalam III Author
Title: Muigizaji Orlando Bloom ampiga Justin Bieber sababu ya demu, sasa dogo anasa mrembo mwengine
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Justin Bieber amerudi tena kwenye headlines baada ya kuingia kwenye ugomvi na muigizaji wa filamu, Orlando Bloom.  Orlando Bloom & ...
Justin Bieber amerudi tena kwenye headlines baada ya kuingia kwenye ugomvi na muigizaji wa filamu, Orlando Bloom.
 Orlando Bloom & Justin Bieber

Ni Orlando ndiye aliyemrushia ngumi Justin Bieber jana huko Ibiza kwenye mgahawa ambao ilimlazimu Justin kuondoka. Mashuhuda wameiambia TMZ kuwa Orlando alikuwa kwenye mgahawa uitwao Cipriani uliokuwa na mastaa kibao Paris Hilton na Diddy.

Kuna watu wanasema kuwa Justin aliongea maneno yaliyomuudhi Orlando kuwa aliwahi kufanya mapenzi na aliyewahi kuwa mke wake, Miranda Kerr.
Miranda Kerr

Miranda Kerr aliwahi kuwa mke wa Orlando Baada ya tukio hilo, Justin Bieber ametumia Instagram kumtupia madongo Orlando ikiwa ni pamoja na kuweka picha yake akiwa analia.

Hata hivyo baada ya Justin Bieberjana kutawala vichwa vya habari baada ya kurushiwa makonde na muigizaji Orlando Bloom kwa ajili ya mrembo Miranda Kerr, ameonesha jinsi alivyo na kisu kirefu zaidi kwa watoto wazuri.
Shanina Shaik na Justin Bieber wakila bata kwenye Yatch

Bieber ameonekana akila bata kwenye yacht katika eneo la Ibiza na mrembo wa Australia anaefahamika kwa jina la Shanina Shaik.

Shanina Shaik ambaye ni mwanamitindo maarufu alipost baadhi ya picha kwenye Instagram akiwa na Justin Bieber.
Shanina Shaik

Mrembo huyo aliwahi kuwa mpenzi wa mwanamitindo maarufu wa Marekani ambaye pia ni muigizaji, Tyson Beckford kwa miaka mingi na uhusiano wao ulivunjika mwaka jana.

Author

Advertisement

 
Top