Mkali wa ‘Pombe Yangu’, Madee amesema muziki wa sasa ni mgumu kutokana
na wasanii kuwa wengi nyimbo nyingi kutoka kwa wakati mmoja.
Madee amesema kurundikana kwa nyimbo kunasababisha kuvipa wakati mgumu vituo vya redio na TV kuzipiga kwa wakati stahiki.
“Sasa muziki unakuwa mgumu kwa sababu nyimbo zipo nyingi sana,” Madee alifunguka.
“Yaani kwa wiki moja zinaweza zikatoka nyimbo nyingi, kwahiyo mpaka nyimbo yako inakuwa kwenye rotation nzuri inatakiwa iwe wananchi wameielewa nyimbo ni nzuri na ni kali na ina sababu ya kuchezwa.
Lakini mimi kwa upande wangu toka nimeanza na ‘Pombe Yangu’ ile kwangu imekuwa rahisi sana kwasababu tayari nimejua ni fanye nini ili kuhakikisha mashabiki hawachoki muziki wangu. Kwahiyo hata wimbo usipofanya vizuri kwa wakati huu najua utafanya vizuri taratibu.”
Habari hii imeandikwa na mtandao wa Bongo5.
Madee