Msanii Davido wa Nigeria amekanusha taarifa zilizosamba hivi karibuni
kuwa amewatenga wasichana wa nchini Liberia sababu ya kuogopa ugonjwa
wa Ebola ambao umeathiri raia wengi nchini humo.
Palikuwa na uvumi kuwa juzi kwenye show ya
Davido nchini Marekani kwenye mji wa Philadelphia, Davido alisema wazi kuwa
hataonekana na mwanamke yeyote wa Liberia sababu hataki kupata virusi
vya Ebola. Davido ametumia twitter na instagram kusambaza ujumbe huu:
Kauli hiyo ilitafsiriwa kama unyanyapaa zidi ya wanawake wa Liberia na Davido amekanusha kuzungumza maneno hayo:
“Tafadhali msiamini tetesi, watu hawana kazi wanatengeneza vitu na kuweka maneno ya uwongo mdomoni mwangu! Sijasema na siwezi kusema vitu kama hivyo” Aliandika Davido.
Davido