Mtalam III Mtalam III Author
Title: Jokate aamua kuingia kwenye Muziki kwa miguu miwili, azungumzia mipango yake
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Kama ulikuwa unafikiria anafanya music for fun basi ujue hauko sawa na mawazo yaliyo kichwani mwa Jokate Mwegelo mwenyewe. Mwanamitindo hu...
Kama ulikuwa unafikiria anafanya music for fun basi ujue hauko sawa na mawazo yaliyo kichwani mwa Jokate Mwegelo mwenyewe. Mwanamitindo huyo ameamua kufunguka wazi wazi kuhusiana na mipango yake ya kufanya muziki.
Jokate

Baada ya kushirikiana na Lucci kwenye Kaka Dada, mrembo huyo amedai kuwa mpango uliopo ni yeye kujitambulisha rasmi kama mwanamuziki kupitia kampuni yake.

“Sasa hivi nataka nijiintroduce kama mimi as a music artist,” Jokate alikiambia kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen ya Kenya ambako alienda kikazi.

“Kwahiyo niwe na single zangu mwenyewe ambazo nazifanyia kazi kupitia kampuni yangu mwenyewe, that’s the way forward.”

Author

Advertisement

 
Top