Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Niiki wa Pili ameanzisha kamtindo ka kutoa Kalamu zake kuhusiana na mambo mbalimbali yanayohusu muziki wa hapa nyumbani.
Diamond na Davido
Hii ya leo inamuhusu zaidi Davido na wasanii wengine ambao wanapiga hela nyingi wanapokuja kufanya shows hapa Bongo. Nikki ana fikra hizi hapa:
Enzi za kina Msondo, Ottu Jaz Band, kina Pepe Kale, Koffi Olomide, Kanda Bongoman, walikuja piga hela Bongo na kuwaacha kina msondo katika umaskini.
Sasa kina Davido wametawala Radio, TV, Clubs, Joints za starehe na wanakuja piga hela nyingi. Air time ya Davido ni ndoto ya wasanii wengi ambao ndio waliotengeneza soko hili.
Karne ya 14 States ndogo ziliungana na kuunda taifa la uingereza ili kulinda soko la ndani na jupigania la nje, hata makoloni ya mwingereza hayakuruhusiwa kufanya biashara na taifa lingine la kizungu.
Baadae marekani states 52 zikaungana na kuwa taifa kubwa lenye soko kubwa la ndani na nje then india, china nao wamefuata theory hiyo nakuwa vizur katika biashara ya utamaduni. Unazani wakati wachina wakivaa vile vinguo katika movie ya BRUCE LEE walikuwa hawoni Timberland, Jeans, Nike na zingine?
Hata Margaret Thatcher na Marekani wakati wanatangaza sera za soko uria na kufungua masoko, wao walidouble ulinzi wa soko la ndani. Wanajua mmoja wa ndani akipata mia wanao mzunguka shilingi haziwezi wapiga chenga…ila mgeni akichukuwa mnabaki na zero.
Hata Margaret Thatcher na Marekani wakati wanatangaza sera za soko uria na kufungua masoko, wao wali double ulinzi wa soko la ndani. Wanajua mmoja wa ndani akipata mia wanao mzunguka shilingi haziwezi wapiga chenga…ila mgeni akichukuwa mnabaki na zero.