Msanii wa Bongo flava, Cpwaa
“Nafungua label yangu..music label yangu kwa hiyo niko sasa hivi na-register wasanii na vitu kama hivyo.” Cpwaa ameiambia The Jump Off ya 100.5 Times Fm.Ameongeza kuwa hiyo itakuwa recording label ya kujitegemea itakayojikita katika kuwasaidia wasanii na kwamba yeye ni mmoja wa member wa label hiyo.
“Ni Brainstorm Music, basically ni recording label ya kujitegemea ambayo itakuwa inasimamia kazi za wasanii nikiwemo mimi mwenyewe niko kwenye hiyo label. Ni kama recording label nyingine za nje ambazo unazisikika sijui Young Money, MMG, Cash Money, Bad Boys kwa hiyo it’s the same thing.” Amesema CPwaa.
“Nimeanzisha label yangu ambayo mimi niko chini yake pamoja na wasanii wengi tu ambao wamekuwa wakinifuata, wakiomba ushauri wakiomba miongozo na misaada ya kifedha. Kwa hiyo wote tutakuwa chini ya uongozi mmoja na shughuli zetu za kisanaa zitakuwa zinashughulikiwa na hiyo label.”
Mwimbaji huyo wa ‘Chereko’ amesema watu wafahamu kuwa hayuko kimya bali yuko busy anajipanga na muda ukifika watamsikia.
Kipindi cha The Jump Off kinakuwa hewani Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili kamili usiku hadi saa nne kamili usiku, na huendeshwa na Jabir Saleh aka Kuvichaka. Habari hii pia inapatikana kwenye timesfm.co.tz (source).