Unaweza kuwa na ndoto za kumshirikisha Young Killa kwenye wimbo wako ambao unadhani anaweza kufit vizuri, Young Killer amezungumza kuhusu muziki wake kwa ujumla ikiwa ni pamoja gharama anazotoza kwenye kushirikishwa.
Msanii wa Bongo flava, Young Killa
Young Killa amesema mpaka sasa ameshaitwa kwenye Collabo nyingi sana lakini anashindwa kufanya kutokana na ubovu wa beats.
Kuhusu pesa amesema hatozi gharama kubwa. Collabo ambazo kafanya mpaka sasa anasema hazizidi tano. Young Killa ameongeza, kwenye collabo zake haangalii mwenzake kaimba nini ila anachokiangalia ni beat na kama ikiwa poa basi anafanya. Habari hii inapatikana kwenye millardayo.com (source).