Msanii wa Bongo flava, Madee
“Ambaye amesaidia kwa msaada mkubwa sana alikuwa ni Ambwene Yesaya (AY), mimi nilimwambia nataka kufanya na Prezzo lakini AY akasema Prezzo kwa sasa hivi ratiba yake haiku vizuri kwa sababu ya habari zake na nini, kwa hiyo tufanye na P-Unit. Na mimi aliponitajia P-Unit nikafurahi, lakini nilikuwa sijawahi kukutana na hao jamaa sasa tutafanyaje, akasema wewe usijali niachie mimi.” Amesema Madee.
Amedai kuwa baada ya hapo, AY alimsaidia kumuunganisha na P-Unit ambapo yeye ndiye aliyesimamia zoezi la kutuma beat Nairobi kwa P-Unit na kisha kuirudisha kwa Marco Chali ambaye alimaliza na Madee. Habari hii inapatikana kwenye timesfm.co.tz (source).