Mtalam III Mtalam III Author
Title: No more beef: Wema na Jokate wamaliza tofauti zao Arusha
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Hatimaye Wema Sepetu na Jokate Mwegelo wameamua kuuzika uadui wao rasmi. Wema na Jokate walishiriki pamoja mashindano ya Miss Tanzania 2006...
Hatimaye Wema Sepetu na Jokate Mwegelo wameamua kuuzika uadui wao rasmi. Wema na Jokate walishiriki pamoja mashindano ya Miss Tanzania 2006 ambapo Wema aliibuka mshindi wa kwanza huku Jokate akikamata nafasi ya pili.
Wema na Jokate kwenye jukwaa moja Arusha.

Uadui wao ulianza baada ya Jokate kuanzisha mahusiano rasmi na mpenzi wa Wema Sepetu miaka kama miwili iliyopita, hapa namzungumzia msanii wa Bongo flava, Diamond. Uhusiano wa Diamond na Jokate ambao ulianza wakati wawili hao wakishoot video ya Mawazo (wimbo wa Diamond) ulienga uadui kati ya Wema na Jokate.

Hata hivyo kuonesha kwamba warembo hao ambao wote wamejikita kwenye usanii wa maigizo, wamemaliza tofauti zao, Jokate alipanda kwenye jukwaa la Divaz Night Endless Fame huko Arusha jumamosi iliyopita na kucheza pamoja na Wema wimbo wa My Number One (Ngololo) wa Diamond. 

Usiku huo ulienda sambamba na Show ya Mirror ambaye ni msanii wa Wema Sepetu. Baadhi ya watu maarufu waliojitokeza kumsupport Mirror walikuwepo Kajala, Martin Kadinda, Wema Sepetu, Jokate na wengine wengi.



Tangazo | Click for more details:

• YS Shower Gels zinauzwa kwa bei nafuu (imported from Malaysia)

Author

Advertisement

 
Top