Japokuwa wimbo wa Cindy Rulz, Lets Wait umetoka miezi michache iliyopita, bado unazidi kukubalika zaidi na kupewa support kubwa na nchi za wenzetu. Mataifa makubwa barani Afrika wanazidi kupagawa na wimbo huo.
Wimbo huo ambao umefanywa na Lamar huku Dunga akiwa ameshirikishwa umekubalika zaidi hasa Nigeria, South Africa, Ghana na kwengineko achana na huko Marekani. Nimepiga story kidogo na Cindy Rulz ili kujua siri ya mafanikio hayo.
Kipindi kile wimbo huu wa Cindy Rulz (Lets Wait) unatoka blogs na webs nyingi zilisupport kwa kushare wimbo huo kwa watu mbalimbali. Lakini ni kwasababu ni wa nyumbani, cha kushangaza nchi zingine za Afrika sasa wanafanya hivyo kwa msanii wetu wa nyumbani Tanzania.
Haya ni baadhi ya maswali niliyomuuliza mrembo huyo anayejua kurap vizuri.
Imekuaje mpaka track yako inafanyiwa sana Promo kwenye Blogs na Webs nyingi za nchi tofauti na Tanzania? Una contacts zao ama nini?
“Contacts sio kihivyo! Nadhani nmewafahamu zaidi baada ya wao kuweka hii ngoma! Yote ilianzia pale walipokua wanamfanyia utafiti Diamond kutaka kujua background yake ya muziki ndo wakakutana na ngoma yangu ya "Let's Wait" lakini wakashindwa kunipata moja kwa moja! Lakini baada ya utafiti zaidi wakaniona Twitter na nikaanza kuwasiliano na baadhi ya watu! Ni vile nikapata contacts chache nawatumia ngoma afu mtu anakua aahh kumbe ndio wewe nilikua nakutafuta ngoma kali na nini! Hivy ikanirahisishia zaidi”
Unahisi ni kwanini wameuelewa sana wimbo wako? Naona nchi kama Nigeria, SA, Ghana na nchi zingine wameonesha support ya kutosha, unahisi ni kwanini?
“Ni wimbo tofauti sana!! Naweza sema kitu tofauti na kitu ambacho hakiko hot kwenye hiphop kwa sasa! Ni wimbo ambao umetulia kiasi cha kwamba hata kama huelewi Kiswahili utakuchukua!! Nakumbuka kuna blogger mmoja marekani aliusifia akisema ni kitu alichokua amekimiss kwenye game na huu wimbo ulimrudisha miaka ilee ambayo wasanii kama kina MC Lyte ndio walikuwa wanavuma au kwa sasa kusema "walikua wanakiki"”
Una Management? Na kama ipo inafanya kazi ya kuhakikisha unaenda level za kimataifa?
“Hehe management?? Sina uhakika na hilo! Sidhani hata kama bongo tunaelewa managers wanatakiwa wanafanyaje! Nachoweza sema ni kwamba naipush ngoma mwenyewe na msaada nikipewa na Lamar. Sio kwa ubaya, nasema tena ni ananisaidia! Ila hizi links na nini ninahustle mwenyewe na kusimamia kazi zangu mwenyewe! Ila kwa upande wa support kubwa sio lamar tu kuna baadhi ya watu pia wananipiga tafu pale wanapoweza...”
Na hii nafasi ya kuweza kusikika kwenye mataifa hayo umeichangamkiaje?
“Na kwa swali lako lingine, naweza kusema kwamba najitahidi kukeep up na hawa watu! Vile nimepata contacts nao nawasiliana tu kawaida na sio mpaka pale ninapokua na nyimbo tu na pia naruhusu wanishauri kwasababu kama jana nlikua nawasiliana na blogger wa Nigeria akanitumia nyimbo ya msanii flani kule akasema kwanini usifikirie kufanya kazi na huyu?? Unaona sasa? Lakin kama ningekua nimejiweka niko juu na nini hata hayo mawazo asingenipa!”
Vipi kuhusu video ya huo wimbo? Naamini itakutangaza zaidi, au unaipotezea?
“Nahisi kila nikiwaza hiyo naugua! Nataka kufanya kichupa kikali kinachoendana na quality ya wimbo au hata zaidi! Nisingependa kufanya kichupa kibovu halafu kikaishusha hadhi ya wimbo”
Wimbo wa Lets Wait umekupa mafanikio gani tofauti na nyimbo zako zilizopita?
“Connections mpya Afrika na nje ya Afrika, nimefahamiana na baadhi ya wasanii nje ya Tanzania ambao wangependa tufanye kazi na pia imeniongezea fan base”
Kwa mfano ukitoa wimbo mwingine utataka kuzingatia nini ili uzidi kwenda level za mbali?
“Quality ya production ya wimbo!! Delivery iwe poa! Hata kama nitabadilisha flows basi utamkaji wa maneno usikike poa! Na pia nicarry emotions kwenye wimbo! Kwamba ukiwa wimbo wa kuparty basi hata ninavyodeliver mashairi nionekane nipo kwenye mood nzuri.
Nakumbuka mtu aliniulza kwa nini kwenye Let's Wait kuna sehemu kama nimecheka kidogo hivi kwenye verse na aliuliza kama nilipanga au ilitokea tu!? Nikamjibu kwamba kila kitu kwenye ngoma zangu nakua napanga najua nitafanyaje! Yote hayo ni kwasababu ninacarry emotions kwenye nyimbo zangu na pia nisimchoshe msikilizaji na unaweza ukaona hili hata kwenye "Utanifanya Nighairi" nilikua narap kwa kufoka kidgo n kihasira ili ioneshe kama kweli nimechoshwa na mapenzi na kweli naweza kughairi!”
Mwisho.
Cindy Rulz bado anaendelea kuja na projects zingine kama kawaida you gotta stay tuned! Baadhi ya shows ambazo kashafanya tangu atoe Lets Wait ni kama urban fresh, Bills, poetry addiction na zingine kibao. Binafsi hii ya poetry addiction imenipa raha sana.
Msanii wa Bongo flava, Cindy Rulz