Mtalam III Mtalam III Author
Title: The ‘Epiq Bongo Star Search 2013’ Winner is Emmanuel Msuya
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Hatimaye kitandawili cha nani atazinyakuwa million 50 za Madam Rita kimetengeliwa jana usiku ambapo mshiriki wa EBSS 2013 kutoka Mwanza, Em...
Hatimaye kitandawili cha nani atazinyakuwa million 50 za Madam Rita kimetengeliwa jana usiku ambapo mshiriki wa EBSS 2013 kutoka Mwanza, Emmanuel Msuya ameibuka mshindi na hivyo kuzimiliki fedha hizo.
Emmanuel Msuya ambaye alikuwa anauwakilisha mkoa wa Mwanza, lakini ni mkaazi wa mji wa Musoma, Mara alitangazwa mshindi wa shindano hilo baada ya kupenya top 3 iliyowahusisha Melisa John, Elizabeth Mwakijambile na yeye mwenyewe.

“Nilikuwa siamini kabisa kama ntakuwa mshindi kwa kweli, lakini namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha. Nawashukuru wote walionisapoti na wote walionipigia kura.  Kwa kweli nafurahi kuona hii ni mara ya kwanza kwa mshiriki toka Mara kushinda.” Msuya aliiambia tovuti ya Times FM muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa shindano hilo.

Alisema anafurahi kuuwakilisha mkoa wa Mara kwa kuwa wengi walikuwa wanaufahamu kwa sifa mbaya za ukatili, lakini sasa wataufahamu kwa kuwa na vipaji vizuri vya waimbaji.

Msuya aliingia fainali na Elizabeth Mwakijambile aliyeonesha ushindani mkubwa. Hata hivyo uwezo wa mkubwa alioonesha Emmanuel Msuya kuimba wimbo wa ‘Maneno Maneno’ wa Ben Pol uliibua shangwe kubwa katika ukumbi wa Escape 1 kitu kilichoashiria kuwa mwimbaji huyo ameweza kuutendea haki wimbo huo na kuwakosha watazamaji huenda kama ilivyokuwa kwa Walter Chilambo mwaka jana.

Msuya alifunika vyema kwa kuimba vizuri ‘Kitambaa Cheupe’ ya King Kiki’, ‘Mapenzi Kitu Gani’ na ‘Maneno Maneno’ ya Ben Pol.

Source: Times Fm Blog


Matangazo | Click them for more details:

• Simu aina ya HTC Desire S ‘S510E’ inauzwa kwa bei nafuu
• Tablet aina ya ‘Swag Tab - Expert 102’ Inauzwa kwa bei nafuu
• Simu aina ya ‘Nokia N9’ Inauzwa kwa bei nafuu

Like Keezywear on Facebook!

Author

Advertisement

 
Top