Mtalam III Mtalam III Author
Title: Mwigizaji Paul Walker wa ‘Fast & Furious’ amefariki kwa ajali ya gari
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Kwa mujibu wa REUTERS, Muigizaji kutoka katika filamu za FAST & FURIOUS ajulikanaye kama PAUL WALKER, alifariki katika ajali ya gari ja...
Kwa mujibu wa REUTERS, Muigizaji kutoka katika filamu za FAST & FURIOUS ajulikanaye kama PAUL WALKER, alifariki katika ajali ya gari jana mchana saa 6:30 NOV 30 huko LA Southern California Marekani akiwa na rafiki yake ambaye naye alipoteza maisha papo hapo.
Mpaka sasa sababu zinazotajwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi uliopelekea gari ikakosa mwelekeo na kupinduka vibaya baada ya kugonga kingo za barabara. Mashuhuda wa ajali hiyo wanadai kuwa baada ya gari hilo lililokuwa likiendeshwa na rafiki wa Paul Walker, lilianza kushika moto na kuteketea baada ya abiria kuwa wameshatolewa ndani ya gari hilo.

Paul Walker amefariki akiwa na umri wa miaka 40 huku filamu ya FAST & FURIOUS toleo la 7 ikiwa katika maandalizi ambayo yeye pia alikuwa muhusika mkubwa. Na kupitia account yake ya Twitter, jana uliwekwa ujumbe wa kuthibitisha kifo cha muigizaji huyo mwenye kipaji na uwezo mkubwa.

"Sadly, I must confirm that Paul did pass away this afternoon in a car accident," Ujumbe huu uliwekwa na Ame Van Iden, Msemaji wa Walker.

Idara ya usalama barabarani ya Los Angeles (County Sheriff's Department) walithibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la Valencia, jijini Santa Clarita, kwenye mida ya 3:30 p.m. (6:30 p.m. ET). Tazama picha za Gari hilo baada ya kupata ajali hapa.

R.I.P Paul Walker!


Matangazo | Click them for more details:

• Simu aina ya HTC Desire S ‘S510E’ inauzwa kwa bei nafuu
• Tablet aina ya ‘Swag Tab - Expert 102’ Inauzwa kwa bei nafuu
• Simu aina ya ‘Nokia N9’ Inauzwa kwa bei nafuu

Like Keezywear on Facebook!

Author

Advertisement

 
Top