Lile kundi la muziki wa Bongo Flava ambalo lilitikisa sana kipindi cha nyuma, Parklane sasa linarudi tena kwa kishindo kikuu. Parklane ambalo linaundwa na Cpwaa na Suma Lee linakumbukwa zaidi na ngoma ya Aisha Aisha.
Baadae Suma Lee na Cpwaa waliamua kufanya Projects zao binafsi kwa miaka kadhaa na sasa wameamua kulirudisha kundi. Akiongelea kuhusu kurudi kwa kundi hilo Cpwaa alisema:
“Habari za Parklane kurudi ni kweli na hivi inavyoongea tayari tumeshaingia studio na tumesharecord aah kuna ngoma ambayo ilitakiwa itoke kabla ya Ramadhani lakini kuna matatizo ya kiufundi yalijitiokeza kwasababu ile ngoma ilikuwa inaenda kurekebishwa halafu studio ambayo imefanyika ni pale A.M pale kwa Manecky, kwahiyo kukawa na delay fulani. Nategemea mwezi huu au ujao tutaachia ngoma.”
Cpwaa pia aliweka wazi kwamba yeye na Suma Lee hawakugombana ila waliamua kufanya kilamtu kazi zake kitu ambacho kimewapa pia mafanikio.
Alipoulizwa kama kuna mtu yukonyuma ya project ya kulirudisha kundi lao, Cpwaa hakuwa tayari kumtaja mpaka pale watakapomaliza kusaini mkataba, ila ametuhakikishia tuu kwamba washikadau wazuri tuu kwenye muziki.
Home
»
Cpwaa
»
Parklane
»
Suma Lee
» Cpwaa na Suma Lee kuirudisha ‘Parklane’ baada ya kimya kirefu sana
Author
Get full package of News, Fashion, Music and Gossip from Tanzania and all over the World! You can also advertise your products, publish your Articles and so much more on Keezywear Blog. Just feel free!