Mtalam III Mtalam III Author
Title: Fuse ODG awachana BET Awards na kugomea kwenda kushiriki kwenye ugawaji wa tuzo hizo
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Msanii anayeitikisa Afrika kwa ngoma zake kali kama Azonto, Antenna na zinginezo, Fuse ODG ambaye alikuwa kwenye kipengele cha Best Intern...
Msanii anayeitikisa Afrika kwa ngoma zake kali kama Azonto, Antenna na zinginezo, Fuse ODG ambaye alikuwa kwenye kipengele cha Best International Act: Africa kwenye Tuzo za BET 2015 aligoma kuhudhuria tukio hilo lililofanyika jana.

Akifunguka kupitia mtandao wa Twitter, Fuse ODG alisema wasanii wa Afrika wanafanyiwa dharau na kituo hicho cha TV ambacho ndio kimeandaa Tuzo hizo. Hii hapa tweet yake akiwafungukia kwanini hakutokea kwenye tukio lile.

Mwaka jana ambapo tuzo hiyo ilichukuliwa na Davido, msanii wa Bongo flava, Diamond alilalamikia kitu hicho hicho ambacho Fuse ODG anakilalamikia sasa! Tatizo kubwa ni kwamba ugawaji wa Tuzo hizo kwenye kipengele hicho hufanyika asubuhi huku ukumbi ukiwa mtupu wakati tukio lenyewe linafanyika jioni.

Author

Advertisement

 
Top