Diamond anawania vipengele vitatu kwenye tuzo za MTV zijulikanazo kama MAMA, na pia bado wimbo wake ambao amemshikisha mkali kutoka Nigeria, Mr Flavour, ‘Nana’ unaendelea kufanya vizuri sana kwenye vituo mbalimbali vya TV hapa Afrika.
Diamond ambaye yuko nchini Nigeria akifanya media tour ya kuitangaza single yake mpya ‘Nana’, anatarajiwa pia kutumbuiza kwenye show ya MTV Road to MAMA itakayofanyika Ijumaa hii July 3, jijini Lagos.
Diamond ataungana na wasanii wa Nigeria akiwemo Iyanya ambaye ameshafanya naye collabo, Yemi Alade, Phyno, Olamide na wengine..