Mtalam III Mtalam III Author
Title: Nelly ataja chanzo cha ugomvi wake na Floyd Mayweather, 50 Cent anazidi kuuchochea
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Ugomvi wa kutupiana maneno kati ya rapper Nelly na bingwa wa masumbwi duniani, Floyd Mayweather ambao umekuwa kwa kipindi kirefu kupitia m...
Ugomvi wa kutupiana maneno kati ya rapper Nelly na bingwa wa masumbwi duniani, Floyd Mayweather ambao umekuwa kwa kipindi kirefu kupitia mtandao wa twitter sasa chanzo kimefahamika vizuri.
Nelly & Floyd Mayweather

Kwenye mahojiano na ESPN, rapper huyo, Nelly alifunguka kuhusiana na utofauti uliopo kati yake na Mayweather huku akimponda kuhusu elimu ndogo aliyonayo bondia huyo. Sasa Nelly alisema yafuatayo:

“Hii stori imechukuliwa tofauti sana, Floyd ni mtu asiyependa kuambiwa hapana, unajua ni ngumu kuongea na mtu ambaye hajamaliza shule ya Secondari” 

Hata hivyo, inasemekana Nelly alimtongoza mpenzi wa Floyd Mayweather, Shantel Jackson na kuanza nae mahusiano kabla ya mwanamke huyo kuachana na Floyd Mayweather kitu ambacho kinampa hasira bondia huyo. Hasira za bondia huyo zilizidi kuchochewa baada ya rapper 50 Cent kumtania Mayweather kwamba Nelly amemchukua demu wake.

Hii sio mara ya kwanza kwa Bondia huyo kuwa kwenye kashfa ya kugombana na wenzake kisa wanawake, ameshagombana na rapper T.I pia miezi michache iliyopita kisa kikiwa Mke wa rapper huyo.

Flody anazidi kukasirishwa na kitendo cha Nelly cha kumchukua mpenzi wake baaday ya 50 Cent kumtania Mayweather kuwa Nelly kamchukua mpenzi wako

Author

Advertisement

 
Top